Kocha wa makipa wa Young Africans, Razack Siwa amesema ili kuendelea kufanya vizuri kwa klabu hiyo katika michezo iliyobaki katika msimu wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, wanahitaji kucheza kwa mipango.

Siwa ambaye alijiunga na Young Africans miezi mitatu iliopita ametoa ushauri hiyo, ili kufanikisha lengo la kushinda michezo yote iliyosalia katika Ligi Kuu, sanjari na michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC).

Kocha huyo kutoka nchini Kenya amesema wachezaji hawatakiwi kuwa na haraka bali kucheza kwa mipango, ambayo ni njia pekee itakayowasaidia kufikia malengo waliojiwekea.

 “Tusiwe na haraka kwasababu tukiwa na haraka kila kitu kinaharibika,” alisema Siwa na kuongeza kuwa kila kitu kinahitaji mipango na utulivu katika kufanya vizuri.

 “Nashukuru Mungu kwa kuwa tulichopanga kimetimia, lengo lilikuwa kushinda na kuondoka na pointi tatu nategemea tutafanya hivyo pia katika michezo mingine minne iliyobaki,” amesema Siwa.

Young Africans inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara kwa kuwa na alama 61, sawa na Simba SC wanaoongoza msimamo huo, huku timu hizo zikitenganishwa na uwiano wa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Hata hivyo Young Africans imecheza michezo 29, ambayo inaifanya klabu hiyo kuwa mbele kwa michezo minne dhidi ya Simba SC yenye michezo 25 hadi sasa.

Gomes: Kesho mtacheka!
Rais Samia, Mkumbo wafanya uteuzi bodi ya TEMDO