Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, (CCM) Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa msimamo wake kuhusu mabadiliko ya Katiba utakuwa tofauti na ule aliokuwa nao awali kabla ya kuingia kwenye siasa na atafuata maelekezo ya Chama chake.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa  baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa katibu mkuu, Abdulrahman Kinana, Dkt. Bashiru aliyekuwa akitetea mabadiliko ya Katiba amesema msimamo huo aliutoa kwa kuwa alikuwa huru.

“Msimamo wa Halmashauri Kuu ndio chombo kikuu kilichoniteua na inaweza kunifukuza. Kwenye uchambuzi kule nisingeweza kufukuzwa, siwezi kuchambua yale ambayo hayajaamuliwa na vikao, kule nilikuwa huru ndio maana nilikuwa natetea Katiba Mpya,”amesema Dkt. Bashiru

Hata hivyo, Dkt. Bashiru amekuwa akijihusisha katika shughuli zilizoratibiwa na Taasisi kwa muda mrefu pia alikuwa kinara katika zoezi zima la kudai mchakato wa Katiba Mpya.

Watumiaji mitandao ya kijamii kulipishwa kodi kupunguza umbea
Arsene Wenger: Ninahitaji kupewa mtihani mgumu