Mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil, Willian Borges amewataka wachezaji wenzake kucheza kwa kujituma katika mchezo wa fainali ili kuweza kutwaa taji la michuano ya Copa America inayofanyika nchini Brazil.

Hayo yanajiri mara baada ya kuripotiwa kuwa Willian hatokuwepo katika mchezo wa fainali lakini mchezaji huyo amewahamasiha wenzake ambao wanaunda kikosi cha timu hiyo ya taifa ya Brazil cha sasa kinacho shiriki katika michuano hiyo, ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka picha akiwa na wenzake wakiwa uwanjani huku akiambatanisha na maneno yenye hamasa ndani yake.

“Sitoweza kuwasaidia wachezaji wenzangu ndani ya uwanja siku ya jumapili ila nitaendelea kuwaunga mkono kwani wanatakiwa kufikia malengo yetu,” ameandika Willian.

Hivi karibuni Shirikisho la soka nchini Brazil CBF lilithibitiha kwamba mchezaji huyo ataukosa mchezo wa fainali utakaopigwa Julai saba mwaka huu siku ya jumapili dhidi ya timu ya taifa ya Peru kutokana na majeraha ambayo aliyapata kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo ambapo walifanikiwa kuitandika Argentina kwa mabao 2-0.

Video: Waziri agomea kuweka bondi mali za JWTZ, Siri familia kutoa mapadri wanne
Putin awasili Rome na kufanya mazungumzo na Papa Francis