Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa amepata taarifa kuhusu mkanda wa sauti wa mauaji ya mwanahabari, Jamal Khashoggi kupitia CIA uliorekodiwa lakini amesema binafsi hatousikiliza wala kuutazama.

Shirika la ujasusi la Marekani CIA limesema kuwa mwanamfalme Mohammed bin Salman aliamrisha kutekelezwa kwa maujai hayo, japo bado Ikulu ya White House haijathibitisha uchunguzi huo.

Aidha, Saudi Arabia imeziita taarifa hizo kuwa ni za uongo na kudai kuwa bin Salman hakuwa na taarifa yoyote juu ya kutekelezwa kwa mauaji hayo.

“Ni mkanda wa maumivu, ni mkanda mbaya sana na hauvumiliki kabisa, mimi siwezi kuutazama wala kuusikiliza,”amesema Trump wakati akizungumza na runinga ya Fox News.

Khashoggi, alikuwa ni kinara wa kuukosoa utawala wa kifalme wa Saudia. aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia Arabia jijini Istanbul nchini Uturuki Oktoba 2 alipoenda kuchukua karatasi zake za talaka.

Hata hivyo, hata wale wanaomuunga mkono Trump ndani ya Bunge la Wawakilishi wanamtaka achukue hatua kali juu ya mauaji hayo, lakini kutokana na unyeti wa Saudia kama mshirika thabiti wa Marekani katika Mashariki ya Kati kunamfanya Trump kuwa mgumu katika kufanya maamuzi.

 

 

Zomea zomea yamkera Leonardo Bonucci
Diamond amvuta Wizkid Wasafi Festival