Mara baada ya Mwanaziki maarufu nchini Marekani Lady Gaga kutangaza kufuta wimbo aliomshirikisha R,Kelly katika platiform zote za muziki ni baada ya skendo iliyovuma kuhusu kuwanyanyasa wanawake kingono.

Skendo hiyo ya unyanyasi wa kingono inayoendelea kumtafuna nguli wa mziki nchini Marekani R.Kelly, imeripotiwa kuwa msanii huyo alipata shambulio la hofu na kuathiri afya yake siku moja baada ya kuoneshwa ‘filamu ya surving R Kelly’ na  kampuni ya Lifetime.

Chanzo cha kuaminika cha TMZ kimeeleza kuwa muimbaji huyo alitetereka kiafya kiasi cha kutafuta msaada wa kitabibu.

Akiwa bado na skendo ya unyanyasaji wa kingono RKelly aliwekwa chini ya ulinzi na askari wa Chicago jana kufuatia simu ya dharura iliyopigwa ikihitaji msaada wao mara baada ya wasamaria wema kumuona Kellz amesimama na wanawake wawili kwenye jengo la Trump Tower, polisi walifanya mahojiano na wanawake hao ambapo ilionekana hakuna chochote kilichokuwa kinaendelea.

Wanawake hao walitambulika kwa majina Joycelin Savage & Azriel Clary ambapo inadaiwa kuwa wazazi wao waliwahi kuingia kwenye mgogoro mzito na Kellz wakidai amepita na mabiti zao.

Kunguni wageuka tishio Kirando
Atashasta akanusha tuhuma za kuihujumu FASTJET 'Wanamatatizo yao'

Comments

comments