Wagonga nyundo wa jijini London “West Ham United” wanajipanga kuwasilisha ofa ya pauni milioni 16, kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Colombia pamoja na klabu ya AC Milan, Carlos Bacca.

The Hammers, wanaamini kiasi hicho cha pesa kinatosha kumng’oa mshambuliaji huyo ambaye amekua hana mwendelezo mzuri wa kucheza soka lake tangu alipojiunga na AC Milan mwaka 2015, akitokea Sevilla CF ya nchini Hispania.

Meneja wa West Ham Utd, Slaven Bilic ameonyesha dhamira ya kutaka kumsajili Bacca, ikiwa ni sehemu ya kuboresha safu yake ya ushambuliaji ambayo ilipwaya mwishoni mwa msimu.

Hata hivyo kuna wasiwasi wa kukubaliwa kwa ofa hiyo, kutokana na viongozi wa AC Milan kumchukuliwa Bacca kama mkombozi wao, kutokana na tatizo la ushambuliaji lililowasumbua kwa kipindi kirefu.

Aitor Karanka Kutupa Ndoano Kwa Fernando Llorente
Joe Ledley Kucheza Euro 2016

Comments

comments