Meneja wa klabu ya West Ham Utd, Slaven Bilic anaamini kiungo wake kutoka nchini Ufaransa, Dimitri Payet atakuwa gumzo katika kipindi cha dirisha la usajili ambacho kitaanza rasmi mara baada ya msimu wa 2015-16 kufikia kikomo.

Bilic, anaamini suala hilo kujitokeza, kufuatia uwezo mkubwa ulioonyeshwa na Payet, tangu alipomsajili mwaka 2015 akitokea nchini kwao Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya Olympique de Marseille.

Amesema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29, amekua na uwezo mkubwa wa kuisaidia klabu ya West Ham, kufikia malengo yake kwa msimu huu, hali ambayo ilipelekea kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa lake na kuchezeshwa kwenye kikosi cha kwanza wakati wa michezo ya kimataifa ya kirafiki.

Meneja huyo kutoka nchini Croatia, amedai kwamba ni mara chache sana kwa mchezaji kama Payet kuwa mzoezfu katika ligi yenye ushindani kama ya nchini England, lakini kwake imekua rahisi kufuatia kiwango chake kuwa cha hali ya juu.

Bilic, amesisitiza kwamba anajua kwa sasa kuna baadhi ya klabu zinamfuatilia mchezaji huyo, na zitaanza kudhihirisha jambo hilo, utakapofika wakati wa dirisha la usajili.

Hata hivyo ametangaza msimamo wa kutokua tayari kumuuza katika kipindi hicho kwa madai ya kumuhitaji kwa udi na uvumba, kutokana na mustakabali wa kikosi chake kuwa mzuri, katika msimamo wa ligi ya nchini England, ambapo huenda The Hammers wakacheza michuano ya barani Ulaya msimu ujao.

Mpaka sasa Payet ameshaitumikia West Ham Utd katika michezo ishirini na nane na kufanikiwa kufunga mabao manane.

Mesut Ozil Bado Anaamini Arsenal Itakua Bingwa
Woodward Amkataa Kiaina Jose Mourinho