Meneja wa klabu ya West Ham United Slaven Bilic ameendelea kutunisha msulu kuhusu mustakabali wa kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Dimitri Payet.

Bilic ameendelea kutoa msisitizo wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29, kufuatia tetesi za mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG kutaka kumsajili Payet itakapofika mwezi janauri mwaka 2017.

Bilic amesema Payet hatoondoka klabuni hapo na amedhamiria kumsainisha mkataba mpya ambao utawathibitishia mashabiki wa The Hemmers kuendelea kuwa mchezaji huyo mpendwa.

“Mwenyekiti alizungumza nami kuhusu mustakabali wa Payet wakati wa fainali za mataifa ya Ulaya (Euro 2016), na alinihakikishia mchezaji huyu hatouzwa,” Bilic aliiambia tovuti ya whufc.com.

“Tunajivunia kuwa na mchezaji kama Payet kutokana na mchango wake mkubwa ambao anaendelea kuuonyesha klabu kwetu, na ninatarajia kuendelea kuwa naye kwa kipindi kingine kirefu.

“Naamini ataendela kutusaidia kwa msimu huu, na ninatarajia atafunga katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Tottenham!”

Super Mario Balotelli Aitamani The Azzurri
Juanfran: Antoine Griezmann Atacheza Dhidi Ya Real Madrid