Klabu ya Huddersfield Town itakayoshiriki ligi ya nchini England msimu ujao, imefanikisha mpango wa kuwabakisha wachezaji wake watatu kwa kuwasainisha mikataba mipya.

Beki Tommy Smith, kiungo Jonathan Hogg na mshambuliaji Rajiv van La Parra walikua wanawanyima usingizi viongozi wa klabu hiyo iliyopanda daraja ikitokea daraja la kwanza nchini England, lakini mapema hii leo walithibitishwa kusaini mikataba mpya.

Smith mwenye umri wa miaka 25, aliiongoza Huddersfield Town kama nahodha msimu uliopita na kufanikisha mpango wa klabu hiyo kutajwa kama klabu bora ya ligi daraja la kwanza, huku Hogg mwenye umri wa miama 28, akichagiza mafanikio hayo baada ya kupona majeraha ya shingo mwezi Machi mwaka huu.

Van La Parra aliyejiunga na Huddersfield Town kwa mkataba wa jumla, alionyesha kiwango kizuri msimu uliopita, hali ambayo ilianza kuwavitia viongozi wa klabu nyingine za ligi kuu, ambao walionyesha nia ya kutaka kumsajili katika kipindi hiki.

“Wote watatu wamesaini mikataba mipya, tunafuraha kuwafahamisha mashabiki wa Huddersfield Town kuhusu  mafanikio haya makubwa ambayo yamesababishwa na timu yote ya viongozi,” imeeleza taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya klabu hiyo. (www.htafc.com)

Kikosi cha Huddersfield Town kimeweka kambi nchini Ujerumani, na baadae hii leo kitacheza mchezo wa tatu wa kujipima nguvu dhidi ya  klabu ya SV Sandhausen inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humo.

RC Rukwa atoa tahadhari kwa wasimamizi wa fedha za ukarabati shule Kongwe
Frank de Boer Azima Ndoto Za Everton