Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imewahakikishia Wananchi juu ya hatua zake ambazo bado imekuwa ikiendelea nazo kwa ajili ya kushughulikia hoja mbalimbali za Muungano.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa upande serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar jijini Dodoma, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema tayari hoja 14 zimekwishafanyiwa kazi.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM katika Mkutano wa 10 wa chama hicho unaofanyika jijini Dodoma.

Amesema, hoja za msingi na zingine nne ambazo zimebaki zitashughulikiwa ndani ya kipindi kifupi kijacho ambapo pia ameyataja mafanikio ya serikali ya Mapinduzi ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa maboresho kwenye sekta ya utalii.

Aidha, ameongeza kuwa kwa sasa watalii wameongezewa siku za kukaa Zanzibar kutoka sita hadi kufikia siku nane na kwamba miaka mitatu iliyobaki ya utekelezaji wa ilani ya CCM, utekekelezaji wa mambo ambayo bado hayajashughulikiwa ipasavyo utafanyika.

Mapigano DRC yaumiza raia wasio na hatia
Mawakili kukata rufaa hukumu ya maandamano