Mama mzazi wa Mwanamuziki maarufu kutoka nchini Marekani Calvin Cordozar Broadus, Jr aka Snoop Dogg, Beverly Broadus Green amefariki dunia.

Mapema mwaka huu Snoop Dogg aliutumia ukurasa wake wa Instagram kuwaomba mashabiki wake kote duniani kumuombea mama yake wakati akiwa hospitalini. Hata hivyo, haikuwekwa wazi ni maradhi gani yaliyokuwa yakimsumbua.

Beverly Broadus Green alikuwa mwandishi na mwinjilisti ambaye alizaliwa Beverly Tate huko McComb, Mississippi, mnamo mwaka 1951. Aliyekuwa akiishi  Long Beach, California nchini Marekani.

Talaka ilivyonigeuza Kahaba
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 25, 2021