Gwiji wa muziki wa hip-hop kutoka nchini Marekani Snoop Doggy ameweka wazi taarifa ya kuwa anataka kuununua mtandao wa Twitter punde baada ya bilionea Elon Musk kutangaza kusitisha azma yake ya kutaka kuununua mtandao huo wa kijamii, wiki chache tu baada ya kutangaza nia yake ya kuifanya kampuni hiyo kuwa ya kwake binafsi kwa mkataba wa dola bilioni 44.

“Huenda watu wawili wanunue Twitter sasa,” ame-tweet Snoop.

Akitumia alama ya hashtag #WhenSnoopBuysTwitter, alishiriki mambo kadhaa ambayo atayafanya kama mmliki mpya wa mtandao huo wenye mamilioni ya wafuasi duniani kote, akiutaja mpango wa kumpa kila mtumiaji wa mtandao huo alama ya bluu iliyothibitishwa (Verification blue checkmark).

“Kila mtu anapata alama ya bluu. hata roboti zenye majina yenye herufi 10 ambazo zinakufuata DM’s na kutoa tu salamu,” amesema Doggy.

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 50, ambaye hivi karibuni alifanikiwa kuingia kwenye headlines za umiliki wa Death Row Records, ameeleza pia mpango wa kuteua bodi yake ya wakurugenzi akiwemo Jimmy kutoka Fish Fry, Tommy Chung, na Pete Najarian.

Licha ya machapisho kadhaa ya rapa huyo kwenye mtandao wa Twitter, akiweka bayana suala hilo, bado haijafahamika kwa undani zaidi ikiwa anadhamira ya dhati ya kuinunua Twitter baada Bilionea Elon Musk kutangaza kusitisha kwa muda mchakato wake wa kuununua mtandao huo.

Musk alisema kwamba mpango huo wa Twitter “umesitishwa kwa muda” alipokuwa akikagua idadi ya akaunti bandia au taka, ambayo Twitter inasema ziko chini ya 5% ya watumiaji.

Inadaiwa kuwa baada ya tweet ya Musk, kuhusu makosa aliyoyabaini katika mtandao huo, hisa za Twitter zilishuka hadi 26% katika biashara ya soko kabla ya hisa kuongezeka tena Saa kadhaa baadae.

Saa mbili baada ya Tweet ya kwanza, Musk alisema yuko tayari kujitolea kukamilisha ununuzi huo.

Ujerumani na Tanzania kulinda hifadhi ya bahari ya Hindi
Mgodi wa Shanta kuanza kuzalisha Dhahabu 2023