Rais wa Chama cha Soka nchini Ujerumani -DFB- Wolfgang Niersbach amejiuzulu kwa tuhuma za ukwepaji wa kodi na kujihusisha na rushwa.

Inadaiwa maafisa wa DFB walitumia njia za rushwa wakati wa mchakato wa kuipa Ujerumani nafasi ya kuwa wenyeji wa kombe la dunia 2006, huku nguvu kubwa ya kufanya hivyo ikitajwa kutoka kwa Wolfgang Niersbach.

Mwanzoni mwa juma lililopita, jeshi la polisi mjini Frankfurt lilivamia makao makuu ya chama cha soka nchini Ujerumani kwa uchunguzi wa madai ya ukwepaji kodi.

Chama cha soka cha Ujerumani (DFB) kilikana madai hayo mwezi uliopita na Wolfgang Niersbach aklisisitiza kushiriki katika jitihada za kupata nafasi ya kuiwezesha nchi hiyo kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2006, kuanzia siku ya kwanza mpaka nyaraka za mwisho huku akikanusha kuhusika na suala la mlungula.

Niersbach alisema alipenda kuweka wazi kila hatua iliyokua inapitiwa katika mchakato wa kusaka nafasi ya uenyeji wa fainali za kombe la dunia, na mambo yote yaliyofanyika yalionekana dhahir.

Kiongozi huyu pia amesisitiza kwa kusema yeye alichukua wajibu wa kisiasa kwa ajili ya malipo yaliyowasilishwa FIFA yenye thamani ya Euro million 6.7 sawa na Pauni million 4.9.

Mbali na kufanywa kwa uchunguzi kwenye ofisi za chama cha soka, pia polisi walifanya hivyo kwenye nyumba za Niersbach, mtangulizi wake Theo Zwanziger, na aliyekuwa katibu Mkuu wa chama hicho Horst Schmid.

Katika taarifa ya Ofisi mwendesha mashitaka imeonyesha kufunguliwa uchunguzi katika madai ya ukwepaji wa kodi kubwa wanaohusishwa na Kombe la Dunia nchini Ujerumani mwaka 2006.

Patrick Vieira Ahamia Marekani
Urusi Hatarini Kufungiwa Na IAAF