Soko kubwa la samaki ulimwenguni linahamishwa kupisha maandalizi ya mashindano ya Olympic yatakayo fanyika mwaka 2020.

Soko hilo lililopo Tokyo nchini japan limekuwa likitumiwa kwa muda wa miaka 83. Soko hilo pia limekuwa kivutio kikubwa sana cha utalii nchini japan kwa ukubwa wake dunia nzima.

Kuhamishwa kwa soko hilo la kihistoria kumekuwa kukipingwa na wanaharakati na wenyeji wa mji huo kwa muda mrefu kabla ya kauli ya mwisho haijatolewa ambayo imeamuru wavuvi na wafanya biashara wote kuhama.

Takribani aina mia tano za samaki walikuwa wana uzwa kila siku katika soko hilo.

Soko hilo lilijengwa mwaka 1935 , baada ya tetemeko la ardhi la mwaka 1923 na lilijengwa imara kwa vyuma ili kujikinga na majanga ya asili yanayo ikumba nchi hiyo kama tetemeko la aridhi.

kila mwaka mamia ya watu hutembelea soko hilo kutalii.

Hadi kufikia tarehe 11 mwezi wa kumi wavuvi na wafanya biashara wanatakiwa kuwa katika soko jipya.

 

Naibu Waziri Kakunda azindua mashindano ya mbio za baiskeli
Mbunge Neema azidi kumwaga misaada Njombe, agusa maisha ya wananchi