Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Borussia Dortmund Michael Zorc, amethibitisha taarifa za beki wa klabu hiyo Sokratis Papastathopoulos kuwa mbioni kujiunga na washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London Arsenal.

Beki huyo wa kati kutoka nchini Ugiriki amekua akihusishwa na taarifa za kuelekea Emirates Stadium tangu mwezi uliopita, na tayari amewahi kuzungumzwa na meneja mpya wa Arsenal Unai Emery, ambaye amechukua nafasi ya Arsene Wenger aliyeondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu wa 2017/18.

Zorc amesema Sokratis ana nafasi kubwa ya kuondoka nchini Ujerumani na kwenda kuanza maisha mengine England, kutokana na mazungumzo baina yao na uongozi wa Arsenal kwenda vizuri.

Zorc ameiambia tovuti na Revier Sport: ‘Kwa asilimia kubwa dili la Sokratis Papastathopoulos linatarajiwa kukamilishwa wakati wowote kuanzia sasa. Kuna baadhi ya mambo tunayaweka sawa kabla ya kumruhusu kuondoka kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.

Klabu ya Arsenal tayari imeshakamilisha usajili wa wachezaji wawili mpaka sasa, ambao ni beki wa kulia kutoka nchini Uswiz Stephan Lichtsteiner akitokea Juventus kama mchezaji huru, na mlinda mlango kutoka Ujerumani na klabu ya Bayer Leverkusen Bernd Leno.

Rais Mnangagwa kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku mbili
Jose Mourinho kuivurugia Liverpool kwa Nabil Fekir

Comments

comments