Kocha wa muda wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer anatarajia mambo makubwa zaidi kutoka kwa mshambuliaji wa klabu hiyo, Alexis Sánchez ambaye alianza kuwasha cheche Ijumaa dhidi ya Klabu ya Arsenal.

Akizungumza na waandishi wa habari, Solskjaer ameeleza kuwa Sanchez ameonesha uwezo mkubwa kuanzia mazoezini tangu alipopewa nafasi ya kuiongoza Man United, na kwamba anaamini mashabiki watafurahia yajayo kutoka kwa mchezaji huyo.

“Sawa, kwa kiingereza changu kibovu na kiingereza chake kibovu… unajaribu kukaa naye chini na kuzungumza lakini ni mchezaji anayechapa kazi, wa kujivunia, na amejikita katika kuonesha thamani yake,” alisema Solskjaer.

“Naamini mashabiki watafurahia zaidi kinachokuja kutoka kwake, amekuwa vizuri tangu mazoezini. Na kiwango chake kimekuwa kizuri sana,” aliongeza.

Sanchez ambaye alihamia Manchester United akitokea Arsenal Januari mwaka jana, alifanikiwa kufunga goli la kwanza dhidi ya klabu yake hiyo ya zamani timu hizo zilipokutana kwenye Kombe la FA Ijumaa iliyopita, ambapo waliwazamisha washika bunduki hao wa London 3-1.

Sanchez alikuwa katika wakati mgumu wa kujitibu majeraha na saikolojia kiasi cha kwenda mapumzikoni nyumbani kwao nchini Chile kwa muda, enzi za kocha Jose Mourinho, lakini ameanza kugeuka lulu akiwa na Solskjaer. Hili lilikuwa goli lake la pili kwa Manchester United tangu Machi mwaka jana.

Baada ya kumpiga Lopez, Thurman amtaka Manny Pacquiao
Mbosso aota kumnunulia Diamond Jumba la Kifahari

Comments

comments