Baada ya kupokea kisago cha mabao mawili kwa sifuri kutoka kwa wagonga nyundo wa jijini London (West Ham United) jana jumapili, meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema ameumizwa na matokeo hayo na wala hakutegemea.

Man United ilikubali kichapo hicho, ikiwa ugenini jijini London kwa mabao yaliyofungwa na Andriy Yarmolenko na Aaron Cresswell, dakika ya 44 na 84.

Solskjaer amesema matokeo hayo ni mabaya na hayakubadiliki kwa ustawi wa klabu hiyo ya Old Trafford.

“Nimesikitishwa na matokeo haya. Siku zote mtu anaumizwa  anapofungwa. ulikuwa mchezo ambao tulipaswa kushinda lakini matokeo yamekuwa tofauti,”alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa timu hiyo.

Meneja huyo kutoka nchini Norway ameongeza kuwa, kikosi chake kina matatizo katika umaliziaji kwa kuwa imekuwa ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini washambuliaji wanakosa umakini.

Kuumia kwa mshambuliaji wake tegemeo Marcus Rashford katika mchezo wa jana, kulionekana kuigharimu timu hiyo kwani ilishindwa kufunga licha ya kupata nafasi.

Solskjaer amesema hana budi kukubaliana na kilichotea jana jijini London, na sasa anajipanga ili kufanikisha lengo la kufanya vyema katika michezo inayofuata.

Hata hivyo, amesisitiza kupokea matokeo hayo kwa mtazamo chanya na anajipanga kukabiliana na changamo zinazoikabili Man United.

Jumatatu Septemba 30, Man Utd itakuwa nyumbani Old Trafford wakiikaribisha Arsenal, katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Ndege yaanguka hifadhi ya Serengeti yaua wawili
Wanafunzi 7 wafariki papo hapo kwa 'kuporomokewa' na paa