Mji mmoja nchini Somalia umepiga marufuku harusi za gharama ya juu ili kuwashinikiza vijana wengi zaidi kuoa ambapo kiwango cha mahari hakitazidi dola 150 (TZS 334,290). Uamuzi huo umetolewa baada ya kubainika kuwa takribani watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa hivi karibuni.

Mohamud Hayd Osman ambaye ni kiongozi wa Wilaya ya Bula Hawa iliyopo karibu na mpaka wa Kenya alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kuaona kuwa kuna ongezeko kubwa la watoto wanaozaliwa nje ya ndoa na hivyo kupata shida ya malezi.

Kamishna huyo ameongezea kwamba gharama ya harusi, ukosefu wa ajira na kiangazi ndio maswala yanayowafanya watu kulihama eneo hilo.

Waandishi wanasema sio kawaida kwa familia ya bwana harusi kutumia takriban dola 5000 katika harusi nchini Somalia. “Mafunzo ya kiislamu yanasema kuwa ndoa inafaa kuwa ya gharama ya chini, alisema Osman.

Amesema wasichana walikuwa wanakataa kuolewa hadi pale kitita cha pesa kitakapotumika kwa dhahabu pamoja na fanicha. (BBC)

Lowassa azidi kulia na njaa
#HapoKale