Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Korea Kusini na klabu ya Totenham Hotspurs Son Heung-min amechaguliwa na Chama cha soka nchini Korea (Korea Football Association (KFA) kuwa mchezaji bora wa nchi iyo kwa mwaka 2020 na kuweka rekodi ya kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya tano.

Msimu huu 2020/21 Son amekuwa na kiwango bora katika klabu yake ya Tottenham inayoshiriki ligi ya Kuu ya England (EPL), akiwa amecheza michezo 12 na kufunga mabao 10, huku akutengeneza nafasi 4 za mabao.

Awali Son alitangazwa kuwa mchezaji bora wa chama cha soka nchini Korea Kusini 2013 kisha aliitetea tuzo huyo mwaka 2014.

Mwaka 2017 alitwaa tena tuzo, alirejea tena kuwa kinara mwaka 2019 na 2020.

Tuzo nyingine zlizowahi kutwaa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ni mchezjai bora wa Bara la Asia mwaka 2018, pia aliwahi kutwaa tuzo ya goli bora nchini Korea mwaka 2015, 2016 na 2018.

JPM: mawaziri na manaibu mmeanza kazi vizuri
Pochettino ajadiliwa Borussia Dortmund