Rapa Soulja Boy amehukumiwa kifungo cha miezi nane jela na siku 265 za kufanya kazi za jamii kwa kosa la kuvunja masharti ya kipindi cha matazamio.

Akiwa mahakamani Jana (Aprili 30), Jaji alimueleza rapa huyo kuwa alikuwa anafikiria kumfunga miaka miwili jela lakini ameshawishiwa na namna alivyoishi kwa siku 40 akiwa nyuma ya nondo hivi karibuni.

Soulja alikuwa anatumikia kipindi cha matazamio pamoja na kufanya kazi za umma kwa kosa la kukutwa na silaha ya moto kinyume cha sheria mwaka 2014. Jaji ameeleza kuwa imebainika hakufanya kazi za jamii kama alivyoelekezwa na kwamba alishirikiana na baadhi ya watu kughushi vielelezo vinavyoonesha kuwa alikamilisha adhabu hiyo.

Februari mwaka huu, Polisi walishtukiza nyumbani kwa Soulja walipokuwa wakifanya uchunguzi kuhusu tuhuma zilizotolewa na mpenzi wake aliyedai rapa huyo alimteka.

Katika ukaguzi wao, polisi walidai kukuta baadhi ya vifaa vya silaha za moto, hatua ambayo ilichochea ugumu wa kupata unafuu.

Wakati huohuo, majanga yameendelea kumuandama rapa huyo kwani alipokuwa jela ndani ya kipindi hiki, kwa mujibu wa TMZ, wezi walivamia nyumbani kwake Agoura Hills, Calif na kuiba pesa taslim $100,000 pamoja na vidani vyenye thamani ya $500,000.

Video: Mwakyembe alinyweshwa sumu, Nataka vyama vingi viendelee - JPM
Adaiwa kumuua mkewe siku chache baada ya ndoa

Comments

comments