Southampton imemsajili beki wa kulia kutoka nchini Ufaransa Jeremy Pied ambaye msimu ulioipita aliitumikia klabu ya Nice.

Pied amesajiliwa na The Saint kama mchezaji huru na sasa anajiunga na mlinda mlango Alex McCarthy ambaye alisajiliwa klabuni hapo saa kadhaa zilizopita.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 27, amesaini mkataba wa miaka miwili ambao utamuwezesha kuitumikia The Saint hadi mwaka 2018, na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha meneja Claude Puel.

Wachezaji wengine ambao tayari wameshasajiliwa na Southampton, ni Nathan Redmond akitokea Norwich pamoja na kiungo Pierre-Emile Hojbjerg akitokea Bayern Munich.

Southampton wataanza mapambano wa kusaka ubingwa wa ligi ya nchini England msimu wa 2016/17, kwa kucheza dhidi ya Watford, Agosti 13.

Nay wa Mitego: Tumemalizana na BASATA, 'Pale Kati' itaanza kuchezwa
FC Barcelona Wasalimu Amri Kwa Montoya, Valencia CF Wachekelea