Kiungo wa klabu ya Leicester City James Maddison, ametajwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England, ambacho mwanzoni mwa juma lijalo kitaanza kambi ya maandalizi ya michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya (Euro 2020).

England watakua wenyeji wa Montenegro Novemba 14 na siku tatu baadae watapapatuana na Kosovo.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate amemtaja Maddison, kwenye kikosi chake, licha ya kukabiliwa na skendo za kupigwa picha akiwa katika Casino, baada ya kuondolewa kikosini mwezi uliopia kwa sababu za kuwa majeruhi.

Kiungo huyo tayari ameshaitwa kwenye kikosi cha England mara tatu, lakini hajafanikiwa kucheza mchezo hata mmoja.

Azam FC, Young Africans katika mtihani mzito

Kocha Southgate amesema anaendelea kutambua mchango wa Maddison na ndio maana anaonyesha kumuamini kwa kumuita kwenye kikosi cha timu ya taifa, na daima hatoyapa nafasi, mambo yaliyowahi kuzungumzwa na vyombo vya habari kuhusu maisha yake binafsi.

“Ninaendelea kupendezwa na uwezo wake anapokua uwanjani, nimedhihirisha hilo kwa kumuita kwa mara ya tatu sasa, japo hajawahi kucheza,” alisema Southgate.

“Mara ya mwisho nilipanga kumtumia katika kikosi changu lakini kwa bahati mbaya alipatwa na majeraha.”

Image result for James Maddison in casinoJames Maddison akiwa Casino.

“Najua baadhi yenu mtakua mmeshangazwa na hatua ya kumuitwa kwenye kikosi kwa kukumbuka tukio lililoandikwa katika vyombo vya habari, binafsi siangalii maisha binafsi ya mchezaji anapokua nje ya soka, hata kama alikua mgonjwa, suala la kuonekana Casino ilikua ni kupenda kwake.”

Kwa upande mwingine kocha huyo amemuitwa beki John Stones, kiungo Alex Oxlade-Chamberlain na mshambuliaji wa pembeni Callum Hudson-Odoi.

England inaongoza msimamo wa kundi A, na kuelekea michezo ya mwezi huu inahitaji alama moja ili ifuzu fainali za Ulaya 2020 (Euro 2020).

Kikosi cha England kilichotajwa kwa ajili ya michezo dhidi ya Montenegro na Kosovo.

Makipa: Tom Heaton (Aston Villa), Jordan Pickford (Everton) na Nick Pope (Burnley)

Mabeki: Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Ben Chilwell (Leicester), Joe Gomez (Liverpool), Harry Maguire (Manchester United), Tyrone Mings (Aston Villa), Danny Rose (Tottenham), John Stones (Manchester City), Fikayo Tomori (Chelsea) na Kieran Trippier (Atletico Madrid)

Viungo: Ross Barkley (Chelsea), Fabian Delph (Everton), Jordan Henderson (Liverpool), James Maddison (Leicester City), Mason Mount (Chelsea), Alex Oxlade-Chamberlain (Liverpool), Declan Rice (West Ham) na Harry Winks (Tottenham)

Washambuliaji: Tammy Abraham (Chelsea), Callum Hudson-Odoi (Chelsea), Harry Kane (Tottenham), Marcus Rashford (Manchester United), Jadon Sancho (Borussia Dortmund), Raheem Sterling (Manchester City) na Callum Wilson (Bournemouth)

Chadema wajitoa uchaguzi Serikali za Mitaa, Jafo awatumia salamu
Magufuli aombwa kuwa mgeni rasmi

Comments

comments