Hatua ya akundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ilifikia tamati usiku wa kuamkia leoa kwa kushuhudia timu 16 zikicheza kwa lengo la kupata ushindi utakaozisaidia kusonga mbele kwenye michuano hiyo, na zingine kusaka tieti ya kushiriki hatua ya mtoano ya Europa League.

Timu zilizomaliza katika nafasi mbili za mwanzo katika kila kundi zimefuzu kucheza hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, na timu zilizomaliza katika nafasi ya tatu zimekwenda kwenye michuano ya Europa League ambayo leo usiku itakua ikimaliza hatua ya makundi.

Katika moja ya michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa usiku wa kuamkia leo, mchezo kati ya majogoo wa jiji Liverpool dhidi ya Spartak Moscow, uliwavutia mashabiki wengi kutokana na kapu la mabao walilobebeshwa warusi.

Liverpool walipata ushindi wa mabao saba kwa sifuri, wafungaji wakiwa ni Philippe Coutinho (matatu), Emre Can, Sadio Mane (mawili) na Mohamed Salah.

Matokeo michezo mingine ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (Uefa Champions League) iliyochezwa usiku wa kuamkia leo.

Real Madrid 3 – 2 Borussia Dortmund

Maribor 1 – 1 Sevilla

Shakhtar Donetsk 2 – 1 Manchester City

RB Leipzig 1 – 2 Beşiktaş

Porto 5 – 2 Monaco

Feyenoord 2 – 1 Napoli

Tottenham Hotspur 3 – 0 APOEL

Liverpool 7 – 0 Spartak Moskva

Trump afanya maamuzi magumu kuhusu mji wa Jerusalem
Video: Hatma Dk. Shika mikononi mwa DPP, Waziri wa JK aeleza machungu ya kulala selo tatu Polisi