Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ametangaza rasmi utaratibu mpya wa kuingia bungeni utakaotumiwa na Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge wakati wanapokuwa wanaingia na msafara na kudai utaratibu huo unaweza kuwasaidia kiusalama zaidi.

Ameyasema Bungeni mjini Dodoma kwenye kikao cha nane, katika mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Utaratibu huu unafaida nyingi, wakati mwingine mnaweza mkawa na hasira tunapopita hapa katikati mkaturukia,”amesema Ndugai

Aidha, Spika Ndugai amesema mlango mkuu wa kuingia Bungeni watautumia kupita endapo kutakuwa na ugeni wa kitaifa kama vile Rais na kufunga au kufungua Bunge na sio vinginevyo.

Hata hivyo, utaratibu huo utakuwa wa kwanza kufanyika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaongozwa na Spika Job Ndugai.

 

Joshua, Wilder watishiana bei kuvunja rekodi ya masumbwi
Mugabe awekwa kikaangoni

Comments

comments