Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameiomba Serikali kufanya haraka uwasilishaji wa mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo waTaifa, kiwango na ukomo wa bajeti.
Ameyasema hayo bungeni muda mfupi kabla ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kuwasilisha mpango huo, Ndugai amesema kuwa kikanuni mpango huo unatakiwa kuwasilishwa Machi 11 ya kila mwaka.
“Kama ikiwa siku hiyo imeangukia siku isiyo ya kazi basi uwasilishaji huu hufanyika siku inayofuata. Mkija mwakani namna hii haitawezekana, hatutakuwa na mjadala,” amesema Ndugai.
Hata hivyo, amewataka mawaziri, makatibu wakuu, maofisa wa Serikali na wabunge kuhakikisha wanakuwapo mjini Dodomahapa kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa mpango huo kisekta na kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakamilika kabla ya kuanza kwa mkutano wa Bunge Aprili 4 mwaka huu

Simba Wakamilika Bukoba, Kuivaa Kagera Sugar J'pili
Ripoti ya Faru John kuwang'oa vigogo wawili