Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa hajapata taarifa yeyote juu ya kuzuiliwa kwa mshahara wa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huku akimtaka Mbunge huyo kuandika barua kwa ofisi ya Spika juu ya madai yake.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na kituo kimoja cha kurushia matangazo kilichopo jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa ukweli ni kwamba hajawahi kusikia chochote kuhusu madai hayo ya mshahara kwamba alimuandikia Spika barua kwamba hakupata mshahara wake.

Aidha, Ndugai amesema kuwa Bunge lina taratibu zake kwani mtu kama hajapata mshahara wake huwa haudaiwi kwenye mitandao bali anatakiwa kufuata taratibu husika.

”Unajua nyinyi mnawafanya wabunge kama Miungu watu, ila wabunge ni watumishi kama wengine wa umma, kama wewe unavyokuwa hujapata mshahara, mbunge naye anatakiwa afanye hivyo hivyo,”amesema Spika Ndugai

Mapema leo Machi 14, 2019, katika mitandao ya kijamii ameonekana Mbunge wa Singida Mashariki akilalamikia juu ya kuondolewa kwa mshahara wake,

 

Zimebaki siku 14 Kamera Daraja la Mfugale "Fly over" kukamilika
Dawa za kutuliza maumivu hatari kwa figo, Dkt Ndugulile afunguka