Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amemtaka Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo kuongeza hoja zake kwani bado ana nafasi katika bunge hilo.

Spika Ndugai alimtaka mbunge huyo wa Jimbo la Arusha Mjini kufanya hivyo, baada ya kuuliza swali la nyongeza mapema hii leo Bungeni mjini Dodoma alilolielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii, ambapo aliitaka Serikali kuona umuhimu wa kusitisha tozo kwa hifadhi zilizo chini ya TANAPA ambazo ziliongezwa ili kutoa fursa ya sekta ya utalii ambayo imethiriwa na Corona.

“Sekta ya utalii kwa mkoa wa Arusha na nchi nzima imeathirika sana wananchi wengi wamekosa ajira, madereva wamekosa ajira kwa sababu magari hayatembei kutokana na uchahche wa ajira, tukiangalia kwenye ukanda wa Afrika Mashariki nchi nyingi zimepunguza tozo. Je Wizara ina mpango gani wa kuipa ahueni sekta ya utalii ili kuweza kunusuru changamoto kubwa ya ajira.” alisema Mrisho Gambo.

Akichangia katika hoja hiyo Spika Ndugai aliongeza kuwa: “Swahi hili lina msingi sana, Mh Gambo bado una nafasi tunaelekea kwenye mipango na bajeti unaweza ukafafanua zaidi hoja yako, ni hoja yenye mvuto na ya msingi sababu haiwezekani graph ya watalii inapungua halafu wewe unaongeza bei”.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Februari 9, 2021
Kichapo cha Namungo FC chamuibua Masau Bwire