Spika wa bunge la Uganda, Rebbeca Kadaaga ambaye pia ni Naibu mwenyekiti wa chama tawala nchini humo (NRM), amemwandikia barua rais Museveni akitaka wanajeshi na maafisa wa polisi walio husika katika kuwapiga wabunge na waandishi wa habari kukamatwa mara moja na majina yao kutajwa hadharani.

Katika barua hiyo kwa rais Museveni, Kadaaga amesema kuwa kinyume na taarifa za maafisa wa serikali kwamba mbunge Bobi Wine hakupigwa, mbunge huyo ana alama zinazo onekana wazi za kupigwa na kuumizwa.

“Rais, ninalazimika kukuandikia barua hii kufuatia vitendo vya maafisa wa usalama kuwapiga wabunge, raia na waandishi wa habari. Maafisa wa kikosi chako cha ulinzi SFC, wanajeshi na maafisa wa polisi walihusika na hadi sasa, hakuna hatua iliyochukuliwa kuwakamata. hatua yao ilivunja sheria dhidi ya dhuluma, ya mwaka 2012, ibara ya 2, 1(a) na (b),” ameandika Spika Kadaaga.

Aidha, Spika Kadaaga amemweleza rais Museveni kwamba iwapo maafisa hao hawatakamatwa, basi itakuwa vigumu kwake kuendelea kusimamia shughuli za bunge.

Hata hivyo, msemaji wa jeshi la Uganda (UPDF) Brig Richard Karemire amesema kuwa jeshi halina kesi yoyote dhidi ya Bobi Wine

 

Hawa Ghasia ajiuzulu nafasi yake CCM
Richarlison aitwa timu ya taifa Brazil