Kampuni ya Kubashiri ya SportPesa imeendelea kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu Sakata la udhamini wake ndani ya Klabu ya Young Africans, ambayo inadaiwa kukiuka mkataba uliosainiwa mwanzoni mwa msimu huu.

Young Africans ilisaini Mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya SportPesa wenye thamani ya Shilingi Bilioni 12,335 lakini mwishoni mwa mwezi Januari ilisaini mkataba mpya na Kampuni ya Vifaa vya Kieletroniki ya Haier kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, ambayo kikanuni Kampuni za kubashiri haziruhusiwi kudhamini Klabu shiriki.

Meneja wa Mahusiano wa Kampuni ya SportPesa Sabrina Msuya amesema, suala la kikanuni kwa klabu shiriki kwenye Michuano ya CAF la kutotumia kampuni ya kubashiri wanalitambua, na walichokifanya ni kushauriana na Uongozi wa Young Africans kabla ya kusainiwa kwa mkataba mwingine na Kampuni ha Haier.

Amesema wakati wakisubiri majibu ya majadiliano waliyozungumza, walishangazwa kuona, Uongozi wa Klabu unatangaza uzinduzi wa Jezi na Mdhamini mpya, ambaye amewekwa kifuani, jambo ambalo kimkataba ni makosa.

“Sisi (Sportpesa) tunajua kuwa hatua ya makundi hatuwezi kukaa kwenye jezi za Young Africans na tulijadiliana cha kufanya ikiwemo kuwapa LiveScore ambayo walisema inahusika na beting na imekataliwa na CAF, tukaomba ushahidi wa maandishi kwa kujua hii inaonyesha matokeo ya mechi na sio kubeti,”

“Wakati tukisubiri kujua cha kufanya tukaona wenzetu (Young Africans) usiku wakizindua jezi na kumtangaza mdhamini mwingine mpya”

“Sisi tayari tumeanza kuchukua hatua ya kuhifadhi haki yake kutoka kwa mamlaka, kwa kuzingatia tuna mkataba na haki ya kuwa kifuani mwa jezi za Young Africans kwa miaka ya soka ya 2022 -2025”

Young Africans ilisaini mkataba kampuni ya Haier wenye thamani ya Tsh bilion 1.5, Jumatatu (Januari 30), jijini Dar es saaam.

Dkt. Mpango, Chiwenga wajadili ushirikiano
Serikali yalaani Wananchi kuvamia, kuuwa Askari