Kikosi cha Tottenham Hotspur kina matumani ya kurejea kwenye uwanja wa White Hart Lane Desemba 26 mwaka huu, tayari kwa mapambano ya ligi kuu ya soka nchini England pamoja na michuano ya kimataifa.

Taarifa zilizothibitishwa na uongozi wa klabu hiyo zinaeleza kuwa, uwanja wa White Hart Lane ambao umefanyiwa maboresho na kuonekana kama mpya, utakua tayari kutumika mwishoni mwa mwaka huu.

Uwanja huo ambao kimtazamo ulikua ukionekana mdogo kabla ya kufanyiwa maboresho kuanzia mwishoni mwa msimu wa 2016/17, kwa sasa upo katika hatua za mwisho na unatarajiwa kuchukua mashabiki 62,062 walioketi.

Mchezo ambao unatarajiwa kutumika kwa ajili ya ufunguzi wa uwanja wa White Hart Lane wenye mtazamo mpya, unatajwa kuwa dhidi ya Bournemouth ambao utaunguruma Desemba 26.

Meneja wa Spurs Mauricio Pochettino amekiri kupokea kwa furaha taarifa za uwanja wao wa nyumbani kuwa katika hatua za mwisho, na wakati wowote mwishoni mwa mwaka watarejea kaskazini mwa jijini London.

Image result for old white hart laneUwanja wa White Hart Lane kabla ya kuanza kufanyiwa maboresho mwishoni mwa msimu wa 2016/17

Meneja huyo kutoka nchini Argentina amesema: “Ni taarifa za kufurahisha sana, tumekua nje ya uwanja wa nyumbani kwa muda mrefu, ninaamini nafasi hii tutaitumia vizuri,”

“Hata wachezaji wangu watafurahia taarifa hizi, kwa maana muda mrefu walionyesha kuhitaji kurejea nyumbani, sasa siku zinahesabika hadi kufikia tarehe maalum ambayo imepangwa rasmi kucheza katika nyasi za uwanja wa White Hart Lane.”

Awali Spurs walitarajia kurejea kwenye uwanja wao Septemba 15, wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Liverpool, lakini zoezi hilo lilikwmaishwa na baadhi ya taratibu za hatua za mwisho za ujenzi ambazo zinaendelea kufanywa uwanjani hapo.

Spurs wamekua wanautumia uwanja wa Wembely kama uwanja wao wa nyumbani tangu mwanzoni mwa msimu wa 2017/18.

Tamko la Kangi Lugola sakata la kutekwa kwa Mo Dewji
Makonda akanusha taarifa za kupatikana kwa Mo' Dewji

Comments

comments