Majeraha ya kiwiko yanayomkabili mlinda mlango wa Tottenham Hotspurs Hugo Lloris, huenda yakamuweka nje ya uwanja hadi mwaka 2020.

Lloris alipatwa na majeraha hayo, wakati wa mchezo wa ligi ya England siku ya jumamosi, ambapo Spurs walikubali kupoteza kwa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Brighton.

Lloris alipatwa na majeraha akiwa katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa langoni kwake na Neal Maupay.

Mlinda mlango huyo kutoka nchini Ufaransa, alilazimika kukimbizwa hospitali, baada ya kupatwa na tatizo la majeraha, na vipimo vimeonesha atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.

Picha za video zimeenesha kuwa, mkono wa Lloris uligeuka nyuma mbele, hali ambayo ilipokelewa kwa masikitiko makubwa na mashabiki wa Spurs ambao siku zote wamekua wakifurahishwa na huduma ya Lloris anapokua langoni.

Taarifa ya klabu imeeleza kuwa: “Hugo Lloris atafanyiwa matibabu ya hali ya juu, baada ya kubainika alipatwa na dhoruba kubwa, akiwa katika mchezo dhidi ya Brighton siku ya jumamosi.

“Hugo atahitaji kupumzika kwa kipindi kirefu, ili kupata wasaa wa kurejea katika hali yake ya kawaida, tuendelee kumuombe katika kipindi hiki kigumu.”

Tayari Lloris alikua ametajwa kwenye kikosi cha Ufaransa, kwa ajili ya michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya (Euro 2020) dhidi ya Iceland na Uturuki, lakini kocha Didier Deschamps amemuita mlinda mlango wa Real Madrid Alphonse Areola kuziba nafasi yake.

“Ni vigumu kuamini kama nitamkosa Lloris, na sielewi atakuwa nje kwa kipindi gani,” alisema kocha Deschamps.

Ulaji chakula kupitiliza husababisha Saratani
Video: Mimba shuleni zamtesa Magufuli, vigogo 13 warudi uraiani