Mmiliki wa klabu ya Leicester City kwa mara ya kwanza amezungumzia maamuzi yaliyochukuliwa dhidi ya aliyekua meneja klabuni hapo, Claudio Ranieri.

Vichai Srivaddhanaprabha ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu hiyo, amesema ilikua ni vigumu kuchukua maamuzi mazito ya kumtimua kocha huyo, lakini ilimlazimu kuafikiana na maazimio ya viongozi wenzake ambao walijadili kwa kina suala hilo.

Amesema ukaribu na heshima kwa meneja huyo kutoka nchini Italia, vilikuwa kikwazo kwake kuafikiana na viongozi wengine wa bodi, kwa kuamini ilikua ni sawa na kumtusi Ranieri ambaye aliwapa ubingwa msimu uliopita.

Hata hivyo, kiongozi huyo amedai ulifika wakati alifumba macho na kuyaafikia maamuzi ya viongozi wengine na kuthibitisha kuondolewa kwa Ranieri, ambaye kwa msimu huu alionekana kushindwa kufurukuta dhidi ya timu pinzani za England.

“Tulifanya maamuzi magumu, hasa kwangu ilinisumbua sana kuafikiana na wengine, lakini ilinilazimu kwa maslahi ya maendeleo ya klabu,”

“Sikutarajia kama kuna siku Ranieri angeondoka kwa namna ile, lakini sina budi kuheshimiana na wengine ili kuona ni vipi tunafanya kazi kwa misingi ya kutimiza makubaliano yaliopo kwenye mikataba ya kazi, na hilo ndilo lilimuondoa Ranieri.” Alisema mmliki huyo kutoka Thailand.

SMZ yakabidhiwa vifaa vya kuboresha huduma za macho
Jamie Vardy: Hakuna Aliyefurahia Kuondolewa Kwa Ranieri