Beki kutoka nchini Senegal Kalidou Koulibaly amemaliza fununu za kutaka kuihama Società Sportiva Calcio Napoli, kwa kukubali kusaini mkataba mpya ambao utamuweka mjini Naples hadi mwaka 2021.

Wakati wa usajili wa majira ya kiangazi Koulibaly, alikua katika mipango ya kutaka kuihama SSC Napoli na klabu ya Chelsea ya England ilionyesha kuwa na nia ya dhati ya kumsajili, lakini msimamo wa viongozi wa Gli Azzurri wa kutaka zaidi ya Pauni milioni 35 kama ada ya usajili ulisaidia beki huyo kubaki Stadio San Paolo.

Koulibaly alijiunga na SSC Napoli mwaka 2014 akitokea nchini Ubelgiji alipokua akiitumikia Racing Genk, na amekua msaada mkubwa katika kikosi cha klabu hiyo inayoshirikiligi ya nchini Italia Sirie A.

Dele Alli Anogewa Spurs, Ajifunga Hadi 2022
Zitto amshauri Magufuli mazito kuhusu Escrow, Muhongo atoa neno