Mlinda mlango kutoka nchini Colombia na klabu ya Arsenal ya England David Ospina amejiunga na SSC Napoli ya Italia kwa mkopo wa muda mrefu.

The Partenopei wamekamilisha dili la kumsajili mlinda mlango huyo, kwa lengo la kuziba nafasi ya mlinda Alex Meret (mlinda mlango chaguo la tatu) ambaye anakabiliwa na majeraha ya muda mrefu.

Ospina ameondoka Arsenal kufuatia shinikizo aliloliweka klabuni hapo, la kuhitaji kucheza mara kwa mara, hasa baada ya kusajiliwa kwa Bernd Leno kutoka Bayer 04 Leverkusen ya Ujerumani miezi miwili iliyopta.

Mlinda mlango huyo ambaye alikuwa miongoni mwa wachezaji waliounda kikosi cha Colombia kilishoshiriki fainali za kombe la dunia nchini Urusi, alihofia kupoteza uwezo wake wa kukaa langoni, kutokana na ushindani uliopo katika kikosi cha The Genners ambapo kwa sasa Leno na Petr Cech wanaonekana kupewa nafasi kubwa ya kuwa kwenye kikosi cha kwanza.

Ospina tayari ameshawasili mjini Naples, na huenda akawa sehemu ya kikosi cha SSC Napoli kitakachocheza mchezo wa ufunguzi wa Sirie A kesho usiku dhidi ya SS Lazio.

BREAKING: Rais Magufuli akiongea na Wananchi Sengerema
Ajichukulia umaarufu baada ya kufanya udukuzi