Mshambuliaji kutoka nchini Poland, Arek Milik amekamilisha mpango wa kuhamia nchini Italia akitokea Ajax Amsterdam ya Uholanzi kwa ada ya Pauni milion 29.6.

Klabu ya SSC Napoli imemuhamishia nchini Italia mshambuliaji huyo mwenye umri 22, baada ya kukunwa na uwezo wake wa kisoka akiwa na timu yake ya taifa pamoja na klabu ya Ajax Amsterdam ambayo aliisaidia kutwaa ubingwa wa Uholanzi msimu uliopita.

Milik, amesajiliwa na SSC Napoli kama mbadala wa mshambuliaji kutoka nchini Argentina Gonzalo Higuain, ambaye juma lililopita alikamilisha mpango wa kujiunga na mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC kwa ada ya pauni milion 76.

Arek Milik, alisajiliwa na Ajax Amsterdam mwaka 2015 akitokea nchini Ujerumani alipokua akiitumikia klabu ya Bayer Leverkusen kwa ada ya Euro milion 2.8.

Kwa msimu mmoja alioitumikia klabu ya Ajax Amsterdam, Milik alicheza michezo 31 na kufanikiwa kufunga mabao 21.

FC Barcelona Wasalimu Amri Kwa Montoya, Valencia CF Wachekelea
Beenie Man aambukizwa virusi vya 'Zika', azuiwa kuingia Canada