Mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans wamefanikiwa kupata matokeo ya sare ya bao moja kwa moja dhidi ya St Louis ya visiwa vya Shelisheli katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Young Africans walikwenda visiwani humo, huku wakiwa na akiba ya bao moja kwa sifuri walilolipata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es salaam majuma mawili yaliyopita.

Bao la mabingwa hao wa Tanzania bara kwa hii leo limepachikwa wavuni na kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajib Migomba katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza, ili hali bao la St Louis limefungwa dakika ya 90.

Hata hivyo sare hiyo ya bao moja kwa moja imeiwezesha Young Africans kusonga mbele kwa jumla ya mabao mawili kwa moja.

Serikali yafuta ada mpya kwenye riadha
Chadema yataka waliokamatwa siku ya maandamano waachiliwe