Mwigizaji wa vichekesho Stanley Yusuph ‘Stanbakora’ ameweka wazi kwamba mwaka huu kama msanii asipobadilika na kuwa mbunifu katika kazi zake atapotea haraka katika soko la sanaa.

Stanbakora alisema kabla ya kutoa kazi zozote mwaka huu wasanii wanatakiwa kufanya tathmini ya walipokosea mwaka jana na kurekebisha makosa hayo kwa kuongeza ubunifu.

”Mwaka tumeuanza vizuri wasanii lakini lazima tujitathmini kwanza tulipokosea mwaka uliopita ili tusirudie makosa na njia pekee ya kufikia mafanikio katika sanaa mwaka huu ni moja tu kuzidisha ubunifu kwa kuwa vitu vingi vimeshazoeleka katika sanaa,” alisema Stan Bakora.

Katika upande wa muziki, Stanbakora hakuonesha wasiwasi nako kwani ushindani ni  mkubwa sana wasanii wanafanyha vizuri sana, shida alionesha upande wa fani ya maaigizo ambako wasanii wengi wameonesha kulala au kuzila fani wakati wasanii wengine kuhama kabisa fani na kujihusisha na mambo mengine.

Hivyo alisisitiza wasanii kuipenda fani yao ya uigizaji na kuongeza ubunifu kwani wao  ndio watakao badilisha muonekano na mtazamo wa fani iyo.

Hivyo aliutunuku mwaka 2017 kama mwaka wa mabadiliko wenye ubunifu wa kila namna kwa wasanii.

 

Video: Lissu 'auziwa' kesi ya Mbunge Chadema, Magufuli apigilia msumali wa moto...
Baada ya kutinga fainali, Azam yamtangaza Kocha Mpya Mromania