Timu ya Stand United imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya kombe la shirikisho Azam Sports Federation Cup (ASFC), kwa kuichapa Njombe Mji bao moja kwa sifuri.

Bao la ushindi la Stand Utd katika mchezo huo uliochezwa mjini Shinyanga kwenye uwanja wa CCm Kambarage, lilipatikana katika dakika ya 12 kupitia Bigirimana Blaise.

Kupoteza mchezo wa hii leo, kunaifanya timu ya Njombe Mji kurejea nyumbani ikiwa na mzigo wa kuanza mikakati ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Aprili 03 dhidi ya vinara wa msimamo wa ligi hiyo Wekundu Wa Msimbazi Simba SC.

Ushindi huo unaifanya Stand Utd kuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho Azam Sports Federation Cup (ASFC), ambayo humtoa muwakilishi wa tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Baada ya Stand kuingia hatua ya nusu fainali, timu zingine zilizosalia kwenye robo fainali ni Young Africans, Singida United, JKT Tanzania, Tanzania Prisons, Mtibwa Sugar na Azam FC.

Wanachama wa chama tawala wavamia kanisa katoliki ‘DRC’
Uingereza yashindwa kupeleka waamuzi kombe la dunia 2018