Mwimbaji nyota wa Nigeria, Dammy Krane ameendelea kusisitiza kuwa Wizkid alimuibia wimbo wake wa Baba Nla.
Dammy Krane ambaye aliwahi kuandika kwenye mitandao ya kijamii na hata kuripitiwa kufanya fujo akidai mshikaji wake Wizkid alimgeuka na kumuibia wimbo, ameiambia Hip TV kuwa hivi sasa mambo yamekwisha lakini bado anaendelea kushikilia msimamo wake.
“Mambo yametulia sasa, lakini kila mtu anajua kuwa Wizkid aliniibia wimbo wangu. Lakini kila kitu kimetuli sasa, tegemeeni ngoma zaidi,” alisema.