Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kuondoka nchini siku ya alhamisi kuelekea Uganda kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo ‘The Cranes’ utakaofanyika Jumamosi,July 4 nchini humo.
Mchezo huo wa marudiano wa kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN 2017 zitakazofanyika nchini Rwanda utachezwa Jumamosi katika uwanja wa Nakivubo jijini Kampala majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Kocha mkuu wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kinaendelea vizuri na maandalizi ya mchezo huo utakaochezwa mwishoni mwa juma nchini Uganda.

“Wachezaji wote waliopo kambini wanaendelea na mazoezi, vijana wanajituma mazoezin, morali ni ya hali ya juu naamini tutafanya vizuri katika mchezo wetu wa siku ya jumamosi” alisema Mkwasa.

Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini alhamisi jioni kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda (Rwanda Air) ikiwa na kikosi cha wachezaji 20, benchi la ufundi pamoja na viongozi.

Aidha, Mkwasa amesema amepanga kuongea na waandishi wa habari alhamisi asubuhi saa 5 kamili, Karume juu ya maandalizi ya kikosi chake.

Stars imeweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo na inafanya mazoezi katika uwanja wa Boko Veterani kila siku jioni kuanzia majira ya saa 10 jioni.

Kila la Kheri Stars, kila la kheri Bon Mkwasa.

Jarida la SA hip hop lamtaja Fid Q kati ya rapaz bora 20 Afrika
Lowassa awashukuru malaki ya waliomdhamini