Uongozi wa klabu ya Inter Milan umemtangaza Stefani Pioli kuwa mkuu wa benchi la ufundi, badala ya Frank de Boer ambaye alitimuliwa klabuni hapo mwanzoni mwa juma lililopita.

Pioli mwenye umri wa miaka 51, amepewa ajira ya kuwa meneja wa klabu hiyo ya mjini Milan, ikiwa bado anakumbukwa kama mtu ambaye alishindwa kufikia malengo ya kukiongoza kikosi cha SS Lazio hali ambayo ilisababisha atimuliwe mwezi April mwaka huu.

Taarifa zilizochapishwa kwenye tovuti ya klabu ya Inter Milan zinaeleza kuwa, uongozi wa klabu hiyo umemsainisha mkataba wa miaka miwiwli meneja huyo kutoka nchini Italia.

Lengo kubwa ambalo Pioli hatakuwa na budi kulifikia ni kuhakikisha Inter Milan inafikia lengo la kufanya vyema katika ligi ya nchini Italia (Serie A) na kufaulu katika hatua ya makundi ya Europa League.

Kabla ya maamuzi ya Pioli kupewa ajira klabuni hapo, majina ya Marcelino na Gianfranco Zola yalikuwa katika mjadala wa viongozi wa juu wa Inter Milan, lakini ikaonekana mzee huyo ana sifa kubwa zaidi ya wawili hao.

Pioli atakuchukua jukumu la kukinoa kikosi cha Inter Milan kutoka kwa meneja wa muda Stefano Vecchi, ambaye alikabidhiwa mamlaka hayo saa chache baada ya De Boer kufukuzwa juma lililopita.

Pioli atafanya kazi kwa usaidizi wa Giacomo Murelli (meneja msaidizi) Davide Lucarelli (Msaidizi wa Ufundi), Matteo Osti pamoja na Francesco Perondi (Makocha wa viungo).

Inter Milan kwa sasa inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi ya nchini Italia, baada ya kucheza michezo 12, wakishinda mara 5, wakifungwa mara 5 na wakitoka sare mara 2.

Breaking News: Trump amshinda Rasmi Clinton, ndiye Rais Mteule
Tovuti ya kampeni ya Donald Trump yadukuliwa