Beki wa pembeni kutoka nchini Italia na klabu ya Man Utd Matteo Darmian huenda akarejea nyumbani wakati wa dirisha dogo la usajili, kufuatia meneja mpya wa Inter Milan Stefano Pioli kuonyesha dhamira ya kumsajili.

Darmian amekua na wakati mgumu wa kujumuishwa katika kikosi cha Man Utd chini ya utawala wa Jose Mourinho,hivyo inaamiwa huenda ikawa njia rahisi kwa Inter Milan kumsajili kwa mkopo itakapofika mwezi januari.

Uwezo wa kupambana wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, unaaminiwa huenda ukatoa changamoto mpya katika safu ya ulinzi ya Inter Milan.

Hata hivyo taarifa nyingine zinadai kuwa, kama Inter Milan watafanikiwa kumsajili Darmian kwa mkopo, huenda wakapendekeza kumchukua jumla itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Man Utd walimsajili Darmian mwaka 2015 akitokea Torino, na mpaka sasa ameshafanikiwa kucheza michezo 30 ya michuano yote.

Alexis Sanchez Kurejeshwa London
Trump atoa kauli za kushangaza baada ya kuteta na Obama kwa dakika 90