Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Stephen Sey anahusishwa na mpango wa usajili wa klabu ya Singida Big Stars, itakayoshiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao 2022/23.

Sey anatajwa kurejea nchini akitokea Misri alipokua akiitumikia klabu ya El Sharkia El Dhokan, kwa madai ya kutolipwa fedha zake za usajili pamoja na mshahara.  

Kabla ya kuondoka Tanzania mwishoni mwa msimu uliopita, Sey alikua akiitumikia klabu ya Namungo FC ambayo aliisaidia kupambana katika Ligi Kuu msimu uliopita sambamba na michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Sey aliwahi kucheza soka mkoani Singida akiwa na Singida United iliyoshuka daraja misimu mitatu iliyopita, hivyo kuhusishwa kwake kujiunga na Singida Big Stars kutamuwezesha kurejea tena mkoani Singida kama dili lake likifanikiwa.

Mbali na Singida Bi Stars kutajwa kumuwania Mshambuliaji huyo, pia klabu ya Geita Gold inayowania kucheza michuano ya Kimataifa msimu ujao, inatajwa kuwa kwenye vita ya kuiwania saini ya Mshambuliaji huyo.

Msomera kumenoga, wahamiaji wasifia juhudi
Balozi Mulamula akataa migogoro ya Jumuia ya Madola