Msanii wa muziki wa hip hop, Stereo ambaye siku za karibuni alitangaza wazi nia yake na hisia zake juu ya kuhitaji kwa udi na uvumba penzi la Chemical.

Stereo amesema ameona itakuwa si vyema ukaisha mwaka 2016 bila kuliweka wazi jambo ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu moyoni mwake kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Stereo alitoa ya moyoni.

”Kiukweli nampenda sana Chemical kutoka moyoni, namzimia muda mrefu hata washikaji zangu wa karibu wanalitambua hilo nasema haya maneno dunia yote ujue kuwa namzimia Chemical, nazungumza haya nikiwa na akili timamu sijalazimishwa na mtu ila ukweli uliopo moyoni mwangu” amesema Stereo kwenye Planet Bongo.

Kupitia kipindi hiko cha planet bongo Chemical naye alijibu live mapigo ya Stereo kufunguka kwa jamii mapenzi aliyonayo kwake.

”Kiukweli nimekuwa suprised (nimepata mshangao) sana kumsikia Stereo sikutegemea kumsikia akizungumza maneno hayo ila anavyozungumza alikuwa akiongea kwa hisia inaonyesha jambo hilo linatoka moyoni mwake,” amesema Chemical.

Ijumaa hii wamekutanishwa live Stereo na mwanadada huyo ‘Chemical’  katika kipindi cha Friday Night Live ambapo Stereo akathubutu kumpigia magoti Chemical kumueleza kile kinachomsibu moyoni mwake.

“Nathubutu kusema ukweli mbele ya umati wa watu wanaotazama hapa muda huu na ambao wanasikiliza kupitia redio wanaona na kunisikia kijana ambaye nampenda Chemical,” Stereo alisema akiwa amepiga magoti pamoja na kumshika mkono mrembo huyo.

“Hii sio siri tena Umma mzima utambue, nipo serious,” aliongeza.

Baada ya kauli hiyo, Chemical alisema “Nimeshakusikia” huku akidai hajawai kupitia experience ya mwanaume kumtokea live namna hiyo.

Mark Noble Afichua Siri Iliyojificha Dhidi Ya Payet
Simone Zaza Atua Mestalla Stadium Kwa Masharti