Mshambuliji wa Man City Raheem Sterling, kwa mara ya kwanza amezungumzia mlolongo wa kuondoka kwake Anfield yalipo makao makuu ya Liverpool.

Sterling aliihama Liverpool wakati wa majira ya kiangazi mwaka 2014, baada ya kugoma kusaini mkataba mpya licha ya kushawishiwa na aliyekua meneja klabuni hapo Brendan Rodgers.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, amesema ilimlazimua kumpa muda wakala wake ili afanikishe azma ya kuachana na Liverpool kutokana na mazingira yaliyokau yakimzunguuka.

“Nakumbuka nilimwambia wakala wangu, juu ya mustakabli wa maisha yangu ya soka, nilimwambia kama sitoweza kutwaa ubingwa nikikwa na Liverpool kwa wakati ule, ni bora akanitafutia mahala pengine ambapo ningeweza kucheza michuano mikubwa barani Ulaya, na kutwaa mataji.

“Bado ninaipenda Liverpool na daima nitaikumbuka kwa mazuri waliyonifanyia tangu nikiwa mdogo, lakini ilinilazimu kuchukau maamuzi ya kuhama kufuatia malengo niliojiwekea.” Amesema Sterling.

Hata hivyo mpaka sasa Sterling ameshafanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya kombe la ligi nchini England (EFL Cup) akiwa na Man City katika msimu wa 2015–16.

Video: Wizara ya ardhi yatoa elimu ya uthamini wa fidia
Video: Swali la Mbowe kwa Waziri MKuu Bungeni