Klabu ya Tottenham imetuma ofa ya Pauni milioni 25, kwenye klabu ya Aston Villa kwa ajili ya usajili wa kiungo kutoka nchini England Jack Grealish.

Spurs wametuma ofa hiyo kwa kuamini itaweza kumshawishi meneja wa Aston Villa Steve Bruce, ambaye anasubiriwa kutoa majibu wa kuibuli ama kuikataa, huku dirisha la usajili wa majira ya kiangazi likitarajiwa kufungwa rasmi kesho Alkhamis.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, amekua katika rada za Spurs kwa muda mrefu, na inaaminiwa huenda safari hii akatimiza ndoto za kuhamika kaskazini mwa jijini London, na kucheza ligi kuu.

Mwanzoni mwa juma hili alikua miongoni mwa wachezjai wa Aston Villa waliocheza mchezo wa kwanza wa ligi daraja la kwanza nchini England dhidi ya Hull City, na kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja.

Baada ya mchezo huo Bruce alisifia uwezo wa Grealish kwa kusema: “Ni mchezaji mwenye kiwango kizuri na ameweza kuisaidia timu kupata ushindi wake wa kwanza msimu huu, ninaimani tutaendelea kumtumia katika msimu huu, na kufikia hatua ya kufanya vyema.

“Tunatambua matamanio ya binaadamu, lolote linaweza kutokea lakini tunaamini ataendelea kuwa nasi ili kufanikia lengo la kupanda daraja na kucheza ligi kuu msimu ujao.

“Viongozi wangu nao wameshaweka wazi mpango wa kutaka mchezaji huyu aendelee kuwa hapa, na hawatokua radhi kumruhusu kuondoka hata kama ofa itatumwa juma hili.”

Kwa hatua hiyo inaonyesha dhahir huenda usajili wa Grealish ukawa na changamoto kubwa, japo lolote linaweza kutokea kutokana na makubaliano yatakayofanywa na  viongozi wa Aston Villa, kufuatia ofa iliyowasilsihwa mezani.

Spurs bado hawajafanya usajili wa mchezaji yoyote katika kipindi hiki cha dirisha la usajili wa majira wa kiangazi, na kama watafanikiwa kumnasa Grealish atakua mchezaji wa kwanza kutua klabuni hapo, kwa ajili ya msimu mpya wa ligi ya England, utakaoanza rasmi siku ya ijumaa.

Rais Kabila kuchukua maamuzi magumu
Video: Lissu narudi nyumbani, CCM waandamana kumpinga mbunge aliyeitosa Chadema