Meneja wa klabu ya Newcastle Utd, Steve McClaren anaangalia uwezekano wa kumrejesha mshambuliaji kutoka nchini England, Andy Carroll kwenye klabu hiyo, ikiwa ni sehemu ya kuhitaji kupangilia mambo ambayo yatainusuru kazi yake kabla ya mwishoni mwa msimu huu.

McClaren, anaangalia uwezekano huo, kutokana na hali ya klabu ya Newcastle Utd kuwa mbaya hadi sasa, ambapo imeonekana kikosi cha The Magpies kinaendelea kujikongoja kwenye nafasi za chini katika msimamo wa ligi nchini England.

Meneja huyo ameonyesha kuwa tayari kuwasilisha ofa ya kumsajili Carroll huko Upton Park magharibi mwa jijini London, yalipo makao makuu ya klabu ya West Ham Utd.

Carroll, mwenye umri wa miaka 26, aliondoka Newcastle Utd mwezi Janauri mwaka 2011 baada ya kusajiliwa na klabu ya Liverpool kwa ada ya uhamisho wa pauni million 35, lakini alishindwa kwenda na kasi ya majogoo wa jiji na hatimae alijiunga na West Ham Utd kwa ada ya paunid milion 15 miaka miwili iliyofuata.

Hata hivyo huenda McClaren, akapata wakati mgumu katika harakati za kulikamilisha jambo hilo, itakapofika mwezi januari mwaka 2016, kutokana na mshambuliaji huyo kuwa sehemu ya mipango ya meneja wa West Ham Utd, Slaven Bilic.

PSG HawaJakata Tamaa Kwa Arsene Wenger
Wa8 Wakamatwa Kwa Uharibu Wa Uwanja Wa Arsenal