Jana mama wa marehemu Patrick, Muna Love alifanya mkutano na waandishi wa habari juu ya msiba wa mwanae ambapo katika maelezo yake alimuhusisha Steve Nyerere aliyekuwa mratibu wa msiba huo kwa upande wa wasanii.

Ambapo Muna alikanusha baadhi ya maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Steve Nyerere kipindi cha msiba huo na kusema hakukubaliana naye chochote kama ambavyo alikuwa anatangaza.

Steve nae kwa upande wake mapema leo hii ameita vyombo vya habari kujibu tuhuma hizo ambapo amesema hakukurupuka kutangaza yale ambayo alikuwa anatangaza kipindi cha msiba wa Patrick na yote aliyoyatangaza yalikuwa ni maagizo kutoka kwa Muna mwenyewe akiwa Nairobi pamoja na mume wake Joel.

”Nikurupuke tu niwatangazie uma wa watanzania kwamba mambo sasa shwari, bila kuambiwa na muhusika mwenyewe bila kuambiwa, kwa akili tu ya haraka haraka, hiyo ni miujiza  gani aliyokuwa nayo Nyerere kupanga ratiba ya watu bila ya kutumwa na muhusika mwenyewe” amehoji Steve.

”Sikukurupuka ndugu zangu, sikukurupuka mi ni mtu mzima nina familia na watoto na ndugu na jamaa, na bahati nzuri nilipewa maagizo hayo na Muna mwenyewe akiwa Nairobi pamoja na mumewe, yule mtu wa nyimbo nyimbo Joel, na wakati ananiambia hivyo niko na baadhi ya ndugu wa Muna” amesema Steve.

Aidha amesema amemsamehe Muna kwa haya yote yaliyotokea kwani anaamini kuwa bado hayupo vizuri.

Pia amemalizia kuwa ”Sifa mojawapo ya kuokoka ni kusema ukweli nalo nimesamehe” Steve Nyerere.

Patrick Aussems kocha mpya Simba SC
Alphonse Areola kumpisha Gianluigi Donnarumma PSG

Comments

comments