Msanii wa maigizo ya vichekesho Steven Mengere maarufu kama Steve Nyerere amesema kuwa msiba wa Patrick ambaye ni mtoto wa msanii mwenzake Muna, utakuwa msiba wake wa mwisho kujitolea kama kiongozi.

Amesema hayo mara baada ya kuambulia maneno ya kejeli na fedheha kutoka kwa watu mbalimbali pindi anapoamua kujitolea kusimamia misiba inayowakuta wasanii wenzake.

“Unajua mimi nina wa­toto, sasa wanapoona ya­nayoandikwa mitandaoni ya kunitukana na kunifedhehesha kwa vitu vya uongo wa­tanichukuliaje, niseme tu huu msiba wa mtoto Patrick Peter ambaye ni mtoto wa msanii mwenzangu Muna ndiyo wa mwisho, sitajihusisha tena na uongozi; kwenye misiba nita­shiriki kama mtu wa kawaida,” alisema Steve.

Steve amesema kufuatia kujitolea kwake katika misiba hiyo amejikuta akiambulia skendo za ajabu kama ulaji fedha za rambirambi na matusi jambo ambalo linamhuzunisha na kuiathiri familia yake.

Cardi B na Offset wamkaribisha duniani mtoto wa kike
Everton, FC Barcelona wamjadili Yerry Mina

Comments

comments