Msanii Maarufu wa Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema kuwa kama si ujasiri wa kiume kuhusu kile kilichotokea wiki chache zilizopita cha sauti yake kuvujishwa na mama wa mwigizaji Wema Sepetu, akisikika akiwataja baadhi ya viongozi kushirikiana naye ili kumsaidia Wema atoke sero, ingemsababishia kifo kwa presha.

Steve Nyerere amesema suala hilo lilimshtua kiasi ambacho aliona kama dunia yote inamwelemea yeye hivyo anamshukuru Mungu kwa kumsaidia kusimama kama mwanaume na kufafanua ukweli wa jambo lenyewe.

“Unajua yale yalikuwa mazungumzo ya kumtoa njiani mama Wema, mpaka nikafikia kuwaweka hadi waheshimiwa Mawaziri mle ndani ya maongezi, ili tu kumpoza yule mama asijisikie vibaya na kuona mwanaye tumemtenga lakini niliposikia yamevuja, nilipata shida sana kuona waheshimiwa watanielewaje?” amesema Steve.

Hata hivyo, Steve Nyerere amesema kuwa amesema kuwa amemsamehe Mama Wema kwa kuvujisha sauti hiyo na sasa anaendelea na maisha yake kama kawaida kwani suala hilo limepita

Tanzanite One yasaidia kikundi cha wanawake madalali Arusha
Video: Waziri Ummy awataka madaktari kuomba ajira Kenya